Monthly Archives: August 2017

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AAGANA NA MGENI WAKE RAIS WA MISRI PIA AKUTANA NA WAZIRI WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN AGOSTI 15,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati wa nyimbo za mataifa mawili zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Rais huyo wa Misri ameondoka mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati akielekea kupanda ndege mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza nyimbo za kikundi cha matarumbeta kilichokuwa kikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi ambaye ameondoka mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

 

 

 

RAIS WA MISRI ABDEL FATTAH AL SISI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI APOKELEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AGOSTI 14,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Agosti 14,2017 Jijini Dar es salaam

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Agosti 14,2017 Jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa wamesimama kwa ajili ya nyimbo za Mataifa yote mawili na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Agosti 14,2017 Jijini Dar es salaam

Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi akikagua gwaride la heshima lililo andaliwa na jeshi la Wananchi kwa ajili ya heshima yake mara baada ya kumpokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Agosti 14,2017 Jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakiangalia ngoma za asili mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Agosti 14,2017 Jijini Dar es salaam